Jinsi ya
kutambua biashara za kimtandao zisizo halali(za kitapeli)
Ajira ni tatizo kubwa linalokabili taifa na
dunia kwa ujumla.Kila mara watu wanafikiria ni njia zipi mtu atazitumia kupata
kipato kitakacho muwezesha kukidhi mahitaji yake pengine na familia yake.Jinsi
gani ya kuongeza kiapato ndo swali gumu ambalo linahitaji majibu,je huyu mtu ameajiriwa au amejiajiri?.Vijana
wengi wanaomaliza elimu zao wanafanya juu chini kujiwezesha na pengine kuajiriwa.Pamoja
kwamba mtu amejiajiri au ameajiriwa bado kuna baadhi yao wanofanya biashara za
kitapeli kama njia ya kujiongezea kipato.Pia idadi kubwa inajitokeza kwa watu
ambao hawajabahatika kujiajiri au kuajiriwa.Baadhi ya watu wamepata pesa nyingi
na pengine kutajirika kabisa kutokana na manbo ya kitapeli.Kitu kinachowafanya
watu wafanye utapeli ni kutokana kwamba hii njia ya kujiingizia kipato isivyo
halali haiitaji nguvu na pia ni rahisi kufanyika.Zipo dalili kadhaa zinazoweza
kukupa ishara fulani juu ya biashara ambayo ni ya kitapeli.Dalili hizi
zitakuwezesha kuhisi kuwa biashara hiyo ina viashiria vya kitapeli.Tuchambua
dalili moja baada ya nyingine;
Mtu kutangaza biashara zake kupitia sehemu za kutolea maoni(comments)
Kama wewe ni mtumiaji mzuri wa mitandao
ya kijamii hususani facebook utakuwa
umeliona au kukutana na suala hili.Sehemu
zenye maoni ndio mara nyingi kukuta matangazo ya aina hii.Matangazo hayo hotelewa
bila yakujali kichwa cha habari cha mada husika.Kwa mfano sehemu watu
walipotolea maoni kuhusu siasa ndipo mtu huweka tangazo lake la biashara ambalo
haliendani kabisa na mada inayotolewa maoni.Lengo la mtu kuweka tangazo lake
hapa ni kupata wateja wa huduma yake na siku zote mtu huangalia sehemu zenye
maoni mengi ndipo huweka tangazo lake hilo.Ndiyo biashara yako inaweza
kutangazwa sehemu ya kutolea maoni lakini je hilo tangazo lako linalingana na
maoni hayo?.Endapo tangazo litatolewa kwenye maoni yahusuyo biashara tajwa basi
hapo hamna tatizo.
Kufanana kwa matangazo yanayotolewa
Matangazo yanayotolewa hususani sehemu za
kutolea maoni (comments) yana fanana fanana.Matangazo hayo ni kama mtu ameyanakili
kutoka kwa mwingine.Maneno na mpangilio wakati mwingine hufanana kabisa na
matangazo mengine kama hayo.Ukiyafuatilia hayo matangazo hayo kwa makini na
kuyafananisha na matangazo maengine ambayo yamesha wahi kutolewa au umeyaona
utangundua kuwa kuna ulinganifu fulani.Mwandishi huyo muda mwingine huchukua
kila kitu kutoka katika tangazo jingine.Ukiataka kungundua hayo chukua
matangazo mawili au matatu ambayo umeshawahi kuyaona na uyafananishe katika
uandishi uliotumika katika matangazo hayo.Kufanana huku kunaweza kusiwe katika
picha tu hata video zilizotumika
zinaweza kufanana.Lakini mara nyingi maneno
huwa ndo yanafanana.
Tangazo kuahidi kupata pesa kwa muda mfupi
Mara nyingi matangazo yanayotolewa na
kumuahidi mtu kupata kiwango fulani cha pesa endapo atajiunga na biashara
hiyo.Tangazo huelezea kwa kina jinsi utakavyoweza kupata pesa na kutajirika kwa
kipindi kidogo tu cha wakati.Tangazo
hilo hutumia lugha ambayo itamuwezesha mtu kuamini kabisa juu ya kilicho
zungumziwa hapo kuwa ni sahihi.Kwa mtu ambaye hajui utapeli juu ya matangazo
hayo akiyapata kwa mara ya kwanza kuna uwezekano kabisa wa kutumbukia katika mikono ya matapeli.Maana
tangazo litamvutia mtu na kumpa hamasa ili tu aweze kupata pesa kwa muda mfupi
kama tangazo lilivyo elezea.Hivyo basi inatupasa kuwa makini na matangazo
yoyote yanayotolewa na kuyapima je ni ya kweli au siyo ya kweli.Ila dalili ya
tangazo kukuahidi kupata kiwango kikubwa cha pesa kwa muda mfupi ni dalili ya
utapeli.
Kutotajwa kwa biashara yenyewe
Hapa unakuta kwamba mtu anaizungumzia
biashara yake lakini hakupi mwanga ni biashara ya aina gani.Huelezea kwa maneno
mengi yenye kumvutia mtu kabisa kujiunga nayo.Katika maelezo atakayotoa hutokuta
anakwambia ni biashara ya vitu gani au inafanyikaje.Kitu pekee baada ya kuelezea
biashara yake atakuambia muwasiliane tu na kuacha taarifa zake za
mawasiliano.Kabla ya kumtafuta mtu ni vizuri uwe na mwanga wa biashara
aliyoitolea maelezo.Mtu huficha taarifa muhimu za biashara kama hiyo ili
kuepuka kugundulika kama anafanya biashara ya kitapeli.Maana akitolea maelezo
ya kukamilika hiyo biashara kwa mtu anaye fahamu basi ni rahisi kugundulika
kuwa hiyo biashara ni ya kitapeli.Hivyo basi hii dalili ni ya muhimu kuichunguza
kutokana na maelezo yatakayotolewa kuhusu biashara hiyo.
Kutolea mifano ya watu waliofanikiwa kupitia biashara hiyo
Kutolea mifano ya watu waliofanikiwa kupitia biashara hiyo
Mwisho kabisa matangazo hayo mengine
hubeba mifano ya watu waliofanikiwa kupitia biashara hiyo.Wakati mwingine asipotaja
watu waliofanikiwa nayo basi mwandishi yeye mwenywewe atasema amefanikiwa nayo
kwa kiwango cha kutosha.Haya yote hufanyika ili kuongezea hamasa kwa mteja
anayetakiwa kujiunga.Mtu akiona kumbe watu wanafanikiwa kupitia hiyo biashara
basi ina kuwa ni rahisi naye kujiunga nayo.Je
maelezo yote yatolewayo ni sahihi au yanaongezewa chumvi tu?.Hizi ni njia
tu za kumshawishi mtu kujiunga na mara nyingi mifano itolewayo inakuwa siyo
sahihi au imeongezewa chumvi kidogo.Usiamini asilimia mia(100%) juu ya taarifa
zinazotolewa labda mpaka nawe uwe na ushahidi nazo.
Hizi ni dalili tu zinzoweza kuashiria
biashara hiyo ni ya kitapeli na siyo kila biashara ikiwa na dalili moja kati ya
hizi ni ya kitapeli.Hizi dalili zinakupa mwanga juu ya kutambua biashara za kitapeli.
Nini maoni yako kuhusu hili?
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni