Njia pekee ya kumuwezesha mtu
kupata kipato chake mbali na kuajiriwa
ni kuanziasha biashara yake binafsi au kujiajiri(ujasiriamali).Ajira ni
changamoto kubwa, kwa kuwa wasomi wanaongezeka na fursa za ajira zipo zile
zile.Kujiajiri kutamuwezesha mtu husasni kijana kupata kipato chake pasipo
kumtegemea mtu mwingine amuajiri.Wazo linakuja ni biashara gani ya kufanya
kumwezesha mtu kupata kipato chake binafsi?Je ni biashara gani yenye mtaji
mdogo?Je hii biashara ya mtandao ni nini?
Ujasiriamali ni uwezo wa kujiajiri
.Unaweza ukawa na wazo zuri la biashara na ukaweza kuliendeleza wewe mwenyewe
au pamoja na kikundi cha watu.Ujasiriamali unaweza kugawanywa katika mafungu
mawili kutokana na fikra zangu;
i.
Ujasiriamali
wa kimtandao(biashara ya mtandao)
ii.
Ujasiriamali
nje ya mtandao
ujasiriamali wa kimtandao
Hii ni biashara ambapo mtu anaifanya
inayotumia chini ya asilimia hamsini za mtandao(50%).Aina hii ya biashara siyo
kwamba mtu hatumii kabisa mtanado bali unakuwa chini ya asilima hamsini.Mfanyabiashara huyu anaweza kutumia mitandao ya kijamii au tovuti zinazofanya matangazo ya
kibiashara.Ila muda mwingi anatumia kufanya biashara yake yeye mwenyewe.Mfano
mfanyabiashara wa duka la nguo atatumia muda mwingi kuuuza bidhaa zake kwa
wateja wake kuliko kuuza mtanandaoni.Vile vile anaweza kutumia fursa ya mtandao
kutangaza biashara yake kufikia watu wengi zaidi.Pia katika biashara hii mfanyabiashara anaweza asitumie mtandao kabisa katika kufanya biashara yake ,mfano
mkulima/mfanyabiashara asiyejua umuhimu wa mtandao.Mfanyabiashara wa aina hii
ni wale wenye fikra kuwa mitandao ya kijamii siyo ya kutangaza biashara
yake.Kutokuwa na mtandao hususani vijijini inachangia mfanyabiashara kufanya
ujasiriamali wake nje ya mtandao.Ujasiriamali huu una faida zake ndo maana watu
wanaendelea kuutumia,je hasara zake ni zipi?
Mfanyabiashara nje ya mtandao
hawezi akaongeza au kupanua soko la bidhaa zake.Hapa tunazungumzia kuongezeka
kwa wateja wa huduma anazotoa mjasiriamali.Kutangaza biashara katika mitandao
ya kijamii pamoja na tovuti kunasaidia kuongeza idadi ya wanunzi wa biashara
yako.Hii inatokana na dhana kwamba idadi ya watu wanaotumia mtandao inaongezeka
siku hadi siku.Uwezekano wa kuapata
wateja nje ya eneo lako ni mkubwa sana endapo mtando utautumia vizuri.
Mfanyabiashara atashindwa
kutoa bei yenye ushindani ya bidhaa zake
kutokana na ushindani uliopo.Kupitia mtandao itakuwezesha kujua bei za bidhaa
kama zako zinazouzwa na wafanyanyabiashra wengine ndani na nje ya eneo lako.Kuangalia
ubora wa bidhaa zinazozalishwa na watu wengine, hivyo kuweka bei kulingana na
bei za wafanya biashara mwengine.Pasipo kujua hayo unaweza kuweka bei ya bidhaa
yako ghali na bidhaa hiyo hiyo mafanyabiashara mwingine akaweka bei rahisi
hivyo ukapoteza baadhi ya wateja.Japokuwa kitu cha kwanza cha kuangalia katika
bidhaa yeyote ni ubora lakini bei pia ina umuhimu wake.
ujasiriamali nje ya kimtandao
Hii ni biashara ambapo mfanyabishara anafanya
shughuli zake zaidi ya asilimia hamsini(50%) mtandaoni.Ujasiriamali wa
kimtandao ni moja kati ya biashara zenye mtaji mdogo kabisa.Hapa mfanyabiashara
anaweza kuwa na sehemu mbili zinazoweza kumuingizia kipato kwa wakati maalumu.Kwanza
kabisa ni sehemu/duka ambalo linauza bidhaa na sehemu ya pili ni mtandaoni.Oda
za manuuzi ya huduma zinafanyika mtandaoni na wanuunuzi wanaenda kuchukua
kwenye duka husika au wanapelekewa kwenye maeneo yao husika.Hivyo mjasiriamali
anakuwa na vyanzo viwili ambavyo vinamletea wateja wa bidhaa zake kwa wakati.Biashara
nyingi zinazo fanyika bila mtandao zitaanza kupungua wateja maana
wafanyabiashara washaanza kutumia fursa bora ya mtandao kuongeza wateja .
Hii ni fursa tosha kutokana na sababu kuwa gharama ya kutangaza biashara katika vyombo vya habari ni kubwa ukilinganisha na mtu atakaye tangaza biashara yake katika mtandao.Pia kupitia mtandao mfanyanyabiashara anaweza kufungua duka la kimtandao ambalo atauza bidhaa zake mwenyewe pasipo kuwa na duka halisi, hapa oda zote na manunuzi yanafanyika katika mtandao na mteja anapelekewa bidhaa alizonununa.Kupitia mtandao utangazaji wa bidhaa zako unawezekana ukawa bure kabisa.
Hii ni fursa tosha kutokana na sababu kuwa gharama ya kutangaza biashara katika vyombo vya habari ni kubwa ukilinganisha na mtu atakaye tangaza biashara yake katika mtandao.Pia kupitia mtandao mfanyanyabiashara anaweza kufungua duka la kimtandao ambalo atauza bidhaa zake mwenyewe pasipo kuwa na duka halisi, hapa oda zote na manunuzi yanafanyika katika mtandao na mteja anapelekewa bidhaa alizonununa.Kupitia mtandao utangazaji wa bidhaa zako unawezekana ukawa bure kabisa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni