Ni kweli kabisa kutokana na tovuti
kuna fursa nyingi ambazo zinaweza kutengenezwa na kuwa biashara.Nafasi hizi
zinatokana na matumizi ya mtandao katika jamii yetu.Vipengele vya kibiashara
vinavyoweza kuanzishwa kutokana na uhifadhi na matumizi ya shughuli za
kimtandao.Ujuzi wako wako, lengo lako na mtaji wako ndio njia pekee itakayokupa
mwanga ni biashara gani ya kuchagua na kuifanyia kazi.Tanzania muamko wa biashara
hizi bado upo chini sana hivyo ni nafasi ya pekee kuchangamkia nafasi hizi za
kujiingizia kiapato.Udogo wa watu katika nyanja kama hizi unatokana na idadi
ndogo ya watanzania wanaofanyia ujasiriamali kupitia mtandao.Endapo utakapo
kusudia kuchukua sehemu mojawapo na kuifanyia kazi basi maendeleo kupitia
kuongeza kipato yanaweza kufikiwa.Kitu cha msingi ni kuepuka kuanzisha biashara
zitazokuwa zikihusishwa na masuala ya utapeli.Ukiepuka hili suala ni kufanya
biashara yako ikue siku hadi siku.Tuangalie hizi fursa kutokana na tovuti;
Hii
ni biashara inayofanyika kwa kutunza au kuhifadhi tovuti.Sio kila kompyuta
inaweza kuzitunza ni kupitia kompyuta maalumu (web servers) ndio tovuti hizi zinaweza
kutunzwa .Vile vile unaweza kutunza tovuti yako kupitia kompyuta yako ya
nyumabani.Gharama ya kuhifadhi tovuti ya mtu inatokana na kiwango cha nafasi na
data atakazotumia vile vile maelewano na mtunzaji wa hizo tovuti.Biashara hii
inahitaji uangalizi mkubwa sana maana
unatunza biashara za watu.Umeme wa uhakika unahitajika vile vile mtandao ambao
lazima upatikane kwa asilimia mia moja na kwa mwaka mzima.Ina maana umeme
ukikatika katika kompyuta unazotunzia basi na tovuti husika haitokuwa mtandaoni
(haitopatikana ukiitafuta).Changamoto ya hapa ni wafanyakazi ambao
watashughulikia mitambo (kompyuta) itakapokuwa na kasoro, umeme unaopatikana
muda wote ,intaneti ya uhakika na kudhibiti uhalifu wa kimtandao katika
kompyuta za kuhifadhia tovuti.Pamoja na hayo kama hauna vifaa hivi unaweza
kupatana na makumpuni makubwa uwe kama mtu wa katikati (affiliate marketer) au
muuzaji wa pili (reseller).Njia hizi mbili zinawezekana kama hauna mtaji wa
kugharamia kompyuta za kuhifadhi tovuti(web servers).Ambapo utatoa huduma ya
uhifadhi wa tovuti bila ya kuwa na wafanyakazi wala kompyuta za kutunzia
tovuti.
Kila tovuti ina jina lake
linaloitambulisha ikiwa mtanadoni.Kuna
aina mbili za majina ya tovuti ,moja
kuna yale yanayotumika kwa dunia nzima ambayo yanaishia na vifupisho kama com,net,org,xyz,design na mengine
mengi.Aina ya pili ni majina
yatumikayo na tovuti zilizo katika nchi husika kama yanayoishia na .tz kwa Tanzania au .ug kwa Uganda.Jina la tovuti yako
linagharamiwa mwaka mpaka mwaka ambapo unaweza kuanzisha tovuti yako ambayo
watu watakuwa wanalipia majina ya tovuti zao.Kwa majina haya yanayotumika dunia
nzima ni vizuri ukawa muuzaji wa kati (affiliate marketer) au muuzaji wa pili
(reseller) wa makampuni makubwa ambayo yanaendesha biashara hizi.Kwa majina
yatumikayo nchini unaweza kuyauza mwenyewe kabisa ila kwa kufuta utaratibu
maalumu uliowekwa.Hivyo basi kupitia kuuza majina haya ya tovuti unaweza
kujiongezea kipato chako.
Hapa
inahitaji uwe na ujuzi wa baadhi ya lugha za kuprogramu tovuti kama vile html, php, javascript, css na nyingine
nyingi.Vile vile kama hauna ujuzi huo zipo programu zitakazoweza kukusaidia
kama adobe dreamweaver, microsoft expression web, adobe muse.Kama
bado haujui kabisa jinsi ya kuandika lugha hizi za kuprogramu tovuti kuna
programu nyingine ambazo zipo katika sehemu za uhifadhi wa tovuti (web hosting
account) ambazo ni rahisi kutumia bila kuwa na ujuzi wa kuandika lugha za kuandika
tovuti.Hizi ni kama vile wordpress, drupal, joomla, blogger na
nyingine nyingi.Hivyo basi biashara hii inawezekana kwa mtu aliye na nia ya
dhati kufanya hivyo na mwenye malengo nayo.Utakapoanzisha huduma yako hakikisha
inatolewa kwa ubora wa hali ya juu ili kuwezesha kukuza jina la kazi
yako.Ukishindwa kutoa huduma iliyo bora basi itakuwa ni vigumu kufanikisha
malengo ambayo ulikuwa umejiwekea kuyakamilisha kwa muda fulani.
SEO
ni kifupisho cha search engine
optimization, ni huduma ambayo utawezesha tovuti ya mteja wako kuonekana
kurasa ya kwanza kabisa katika programu za kutafuta kama vile google ,yahoo na bing .Tovuti yako inapoonekana katika kurasa ya kwanza ya hizi
programu inakuwa ni rahisi kabisa kupata watembeleaji katika tovuti yako.Lengo
kubwa la kufungua tovuti ni kuhakikisha inaonekana kwa watu wengi na walengwa
wa suala hilo.Ili kuhakikisha inaonekana katika kurasa ya kwanza kabisa katika
programu hizi za kutafuta huna budi kuhakikisha tovuti yako inakidhi viwango vinavyotakiwa
vya seo.Bila ya kufuata viwango hivi
tovuti yako haitoweza kuonekana katika kurasa za kwanza hivyo inaweza kusababisha ukakosa wateja au ukapunguza
wateja kakia ujasiriamali wako.Hapa unaweza kupata ajira kwa kutoa huduma hii
kwa watu ambao wanaohitaji.Ukiwa na ujuzi katika sula hili utaweza kujiongezea
kipato kupitia huduma ya seo.Epuka
njia zisizo sahihi (black hat) katika kutoa huduma yako kwa wateja.
Mtu
anaweza kuanzisha tovuti ila suala ya kuitangaza likiawa ni jukumu zito sana. Hapa
kama una ujuzi kuhusu hili huu ndo wakati muafaka wa kuongeza kipato
chako.Ushauri kama wa biashara katika mitandao ni muhimu sana katika kukuza tovuti yako.Jinsi gani uendeshe biashara yako
kupitia tovuti,je ni njia gani utumie kuitangaza biashara yako?. Mtu utumie
matangazo ya kulipia (paid ads), kupitia mitandao ya kijaamii (social media
marketing) au utumie seo (search engine optimization) tu.Vile vile katika
kufanya mauzo ya bidhaa zako utumie njia gani ambazo zitakidhi matakwa ya
watumiaji.Pande hizi mbili ni muhimu kuzingatiwa kuwezesha kukuza kipato cha
tovuti yako.Kama una ujuzi wa mambo kama haya ni rahisi kuongeza mapato yako
kupita watu watakaotaka huduma kama hizi.Hivyo ushauri kupitia kuitangaza tovuti
unaweza kukuwezesha kupata ajira pia.
Una maoni
gani? Andika katika kisanduku cha maoni.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni