Sayansi na teknolojia ni jambo muhimu sana
katika kukua kwa uchumi wa nchi yoyote ile.Maana teknolojia itawezesha kubuni
mifumo ambayo itasaidia watu kufanya kazi kwa ufanisi na kwa muda mdogo.Teknolojia
katika mifumo ihusiyo miamala ya kipesa
ikiwa ndogo ndio chanzo kikubwa cha kuanzisha wizi wa mtandaoa.Watu wenye ujuzi
hutumia mianya katika mifumo hiyo kufanya matukio ambayo yanaweza kusababisha
upotevu wa pesa.Haya yote yanatokana na kwamba teknolojia itumikayo katika hizi
kampuni zenye miamala ya kipesa ni ndogo sana.Vile vile makampuni haya
yanawezekana yasiwe na wataalamu wenye ujuzi wa
kutosha katika kutimiza majukumu yao, au kampuni lina miundombinu isiyokidhi
usalama wa pesa zilizowekwa.Vilevile inawezekana baadhi ya wafanyakazi ndo
wahalifu wenyewe au wanashirikiana na wahalifu hao maana yote haya yanawezekana.Hivyo
makampuni hayo hayana budi kuchukua hatua madhubuti kukabiliana na suala hili.
Hili suala la wizi katika mitandao ya
simu Tanzania linaonekana kukua siku hadi siku.Ambapo mtu anachukua namba za
simu za watu pengine mnaoheshimina nao na kukutumia ujumbe mfupi ambao utakutaka
utume pesa kiwango fulani ila atakurudishia kwa muda ambao atautaja yeye.Je hizi namba
wanazipataje?.Hizi namba zinaweza kupatikana kutokana labda mtu ameibiwa simu
yake au ameiangusha.Vile vile mtu anaweza kukupigia na kujifanya ni mtoa huduma
katika mtandao wako wa simu na kuanza
kukuuliza maswali mengi yahusiyo simu yako.Maswali haya yanaweza kuwa matumizi
yako ya miamala ya pesa katika simu yako, tarehe ya mwisho ya muamala, tarehe
ya kuzaliwa na pengine hata namba yako ya siri.Ila namba itakayokupigia hapo mara
nyingi siyo ya huduma kwa wateja( mfano 100 kwa Vodacom) bali ni namba ya
kawaida tu kama za watu wengine unaowasiliana nao.Mtu akipata taarifa kama hizi
anaweza kuibadilisha laini yako na kuanza kuitumia yeye mwenyewe ,ambapo
anaweza kutoa pesa iliyo kuwepo au kuanza kuwatumia ujumbe watu wamtumie pesa
kwa hiyo namba.Hapo namba yako ikibadilishwa, mtandoa hautosoma katika laini yako na itakuwa
imefungiwa.Tuzingatie haya yafuatayo kuepuka wizi;
Wizi kupitia mitandao pia unaweza
kufanyika kupitia taarifa tunazozitoa kwa watu wasio waaminifu.Hapa wizi huu
unafanyika mara nyingi mtu unapofanya manunuzi au kulipia huduma fulani mtandaoni, ambapo
utatakiwa kuandika taarifa muhimu kuhusu akaunti yako ya benki.Wizi wa ana hii
unaweza kufanyika kwa njia mbili moja ni
kupitia kufanya manunuzi katika tovuti zisizo aminika.Hakikisha unapofanya
manunuzi, katika tovuti unayofanyia manunuzi au kupata huduma fulani inatambulika
vizuri.Maana ukifanya miamala yako katilka tovuti hizi zisizo aminika unaweza
kupoteza pesa zote zilizo katika akaunti yako.Njia ya pili inafanyika kupitia kurasa zisizo halali za tovuti husika.Unaweza
kufanya miamala katika tovuti husika kumbe ile kurasa unayotumia imebadilishwa
bila ya wewe kujua.Hii inawezekana endapo utaambiwa kufanya muamala kupitia
linki utakayotumiwa kupitia barua pepe au ujumbe mfupi.Tufanye haya kusaidia
kuepuka kupoteza fedha zetu;
i. Unapofanya miamala katika tovuti
hakikisha hizo tovuti zinaaminika(trusted sites).
ii. Kuwa makini na miamala unayotakiwa
kuilipia kupitia linki za barua pepe au ujumbe mfupi.
iii. Usindike namba yako ya siri katika
tovuti unazo takiwa kufanya miamala.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni