Pamoja na kuwa na kazi ya kufanya au
kutokuwa nayo inawezekana hauna kipato cha kutosha kitakacho kuwezesha kukidhi
mahitaji yako.Kipato chako ndicho kitakuwezesha kufanya shughuli zako za
kimaendeleo ndani na nje ya familia yako.Kipato cha kutosha kitakuwezesha
kumudu mahitaji ya familia na kufanya shuguli za maendeleo.Endapo kipato chako
kitatumika kukidhi mahitaji ya familia tu bila kufanya shughuli za kimaendeleo
basi unahitaji kuongeza kipato chako.Kuongeza kipato kutakuwezesha kuendelea
mbele na kutotegemea mshahara pindi unapomaliza kazi( kustaafu).
Zipo njia za kuongeza kipato kupitia mtandao
ambazo mtu anaweza kuzitumia na kufanikisha kuongeza kipato chake .Kitu cha
msingi ni kuangalia njia ambazo ni za ukweli na hazina utapeli wowote.Uzuri wa
baadhi ya njia hizi zinazoweza kutumika katika kuongeza kipato ni kwamba unaweza
kuzifanya mbali na muda wa kazi.Njia hizi zinafanya kazi kwa ajili yako ukiwa
katika shughuli zako za kawaida.
Idadi ya watu
wanaotumia mtandao Tanzania inaongezeka siku hadi siku.Hivyo basi hii ni fursa
pekee itakayo muwezesha mtu kukuza kipato chake binafsi.Kama una biashara yako
na ungependa kuongeza idadi ya watumiaji
wa bidhaa zako basi njia bora zaidi ni kufungua tovuti kwa ajili ya biashara
yako.Biashara zinazo fanyika mtandaoni zina asilimia kubwa ya kufanikiwa kuliko zile zisizo tumia mtandao.Utakapo
fungua tovuti yako hapo utakuwa na vyanzo vya wateja vya ania mbili,moja ni
wale wateja wa kawaida ambao hawatumiii mtandao na aina ya pili ya wateja ni ya
wale wanaotumia mtandao kutafuta bidhaa za kununua. Hivyo idadi ya wateja
katika biashara yako itaongezeka.
Tangaza biashara yako katika tovuti za matangazo (classified ads websites).
Kupitia
tovuti zinazotoa huduma ya kuweka matangazo yako ya biashara bure
kama vile kupatana.com na nyingine
nyingi ambazo unaweza kutangaza biashara yako.Tovuti hizi zitakusaidia katika
kuongeza iadadi ya wateja katika biashara yako.Huduma kama hizi anaweza
kuzitumia mtu ambaye ana tovuti yake ya biashara pia ambaye hajafungua tovuti kwa ajili ya
biashara yake.Ukiweka biashara yako katika tovuti hizi basi kuna uwezekano
mkubwa wa kuongeza mauzo kwa ajili ya biashara yako.Ambapo mtu atafanya
manunuzi na malipo yatafanyika kutokana na utaratibu wa tovuti husika.
Anzisha tovuti ya matangazo ya
kibiashara (classified ads website).
Njia nyingine
inayoweza kukuongezea kipato ni kufungua tovuti za kibishara ambapo mtu unaweza
pia kutangaza biashara yako.Lengo kuu la kuanzisha tovuti za kibiashara ni kuwezesha watu kuweka
matangazo yao katika mtandao kiurahisi na kwa muda mfupi.Inakuwa rahisi watu
kutafuta bidhaa wanazo zihitaji katika
hizi tovuti maana watazipata kiurahisi na kuwezesha kulinganisha na bidhaa
nyinginezo zilizowekwa katika mtandao.Kitu cha msingi ni kuwezesha biashara
yako kutambulika kiurahisi na watu wengi hivyo kufanya wepesi wa kuitumia.Hapa
mtu anaweza kuongeza kipato kwa kutangaza baadhi ya matangazo kwa malipo
maalumu kutokana na makubaliano na wateja wake.Watu wengi wanatumia matangazo
yaliyodhaminiwa (sponsored/premium ads) katika kuingizia kipato tovuti zao.
Changamoto inakuja ni jinsi gani ya kuanzisha
hizi tovuti.Je ni kiwango gani cha pesa unaweza kukiweka katika kuanzisha mradi
wako.Ukweli ni kwamba kiasi cha pesa ambacho utakiweka hapa kinatokana ana aina
ya tovuti uitakayo kuianzisha.Kufungua tovuti kama ya matangazo ya kibiashara
ni gharama kidogo ukilinganisha na tovuti za kawaida .Maana katika tovuti hizi
kiwango kikubwa cha nafasi kinahitajika kutunza tovuti yako.Gharama hii utakayo
ilipia ni ndogo kuliko kodi ya chumba
chako cha biashara kwa mwezi mmoja.Pesa hii utayo lipia hapa itakuwezesha
kuendesha tovuti yako kwa mwaka mzima.Lakini tovuti za kawaida gharama yake nia
ndogo ambayo kila mtu anaweza kuimudu na kuanzisha tovuti yake.Haihitaji uwe na
ujuzi na lugha za kompyuta kuweza kufanikisha hili, kuna programu ambazo zipo tayari kabisa kuwasaidia
watu wasiojua lugha hizi za kompyuta kutengeneza tovuti zao.
Una maoni/ushauri kuhusu hili au unahitaji
maoni/ushauri kuhusu hili suala basi andika lolote katika kisanduku cha maoni
vile vile jiunge(subscribe) kupata taarifa pindi tunapoandika makala.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni