Ni kweli kabisa kwamba njia moja wapo itakayokuwezesha
kuanzisha biashara yako ni mtandao.Fananisha
mtandao kama ni shamba kubwa ambapo mtu
unaweza kulima mazao yako, na tovuti ni kama mmea utakaokuwezesha kuvuna
matunda yako (kipato).Utakapotunza mmea wako vizuri ndio utakapopata mazao
yenye ubora.Kufungua tovuti ndio njia pekee itakayokuwezesha kuendesha biashara
yako au huduma zako na pengine kukuingizia pesa .Hiyo utakapokuwa na tovuti
mtandaoni basi ni lazima uifanye kama kitegauchumi kitakacho kuingizia kipato.Ijapokuwa
kufungua tovuti au kufanya biashara ya mtandaoni ni rahisi lakini kuna
changamoto zake.Ni biashara ya aina gani unataka uianzishe ,walengwa wake ni
akina nani, bidhaa gani unataka uwauzie,njia zipi za kuwasambazia?. Vitu kama
hivi ni muhimu kuvijua ili kuweza kufungua tovuti kwa ajili ya biashara yako.
Sio lazima unapofungua tovuti iweze
kukuingizia kipato.Hapa inatokana na lengo lako wewe unafungia kutimiza matakwa
gani.Tovuti zisizo ingiza kipato mara nyingi ni tovuti za kutoa taarifa/habari
kwa jamii kama tovuti za shule na vyuo.Lakini kumbuka mtandao ni soko kubwa
linalokua siku hadi siku hivyo linaweza kutumika kama njia mojawapo ya kukutafutia
wateja.Mbinu na mikakati madhubuti ndiyo jambo la msingi katika kufungua biashara
yako ya mtandao.Utakapofungua tovuti bila ya kujua ni kitu gani unataka ukiweke
,itakuwa ni vigumu kutengeneza kipato chako.Hivyo basi ni njia gani zitakazo
kuwezesha kufungua tovuti yenye mafanikaio?.Fuatilia lengo moja baada ya
linguine katika Makala hii;
Je una
kipaji,biashara au huduma ambayo ni nzuri na watu wanaihitaji?. Hapo ndipo
uanzishe tovuti yako kwa ajili ya hiyo huduma au biashara.Watu siku zote
wanahitaji kupata huduma iliyo bora na isiyo na mashaka yoyote.Utakapoanzisha
biashara yenye thamani itakuwezesha kupata wateja wengi na kwa haraka zaidi.Fikiria
kitu ambacho watu wanakifikiria kukipata kutoka katika huduma fulani na
hawakipati, hapo ndio uanzishe huduma kwa ajili ya kitu hicho watu wasichokipata.Vile
vile ubora wa biashara yako au huduma yako uwe na kiwango kikubwa.Utakapouza au
kutoa huduma yenye ubora basi biashara yako au huduma yako itadumu kwa muda
mrefu zaidi.Hii ndio sehemu ya muhimu kabisa maana watu wanapenda kuona vitu vipya
na vyenye ubunifu ndani yake.Ukifanikiwa katika sehemu hii ya kwanza ya
kutambua huduma au biashara ya kuwauzia watu sehemu zinazobaki zinakuwa ni
nyepesi kufanyika.
Ukishakuwa na wazo au lengo lako toka hapo
awali ndipo sehemu hii ya pili inafuata.Baada ya kutafakari huduma bora ya
kuwapa watu ndipo unapoyaweka mawazo yako katika vitendo.Fungua tovuti kwa ajili
ya wazo lako na yenye mvuto kuwavutia wateja wako.Unaweza kuibuni tovuti yako wewe
mwenyewe au ukamlipa mtu kiwango fulani cha pesa mtakacho kubaliana ili aweze
kukubunia tovuti yako.Pia unaweza kuibuni wewe mwenyewe maana kuna programu
ambazo zinaweza kukusaidia kubuni tovuti yako bila kuwa na utaalamu wa lugha za kompyuta.Chaguo ni lako ila lengo
ni kuwezesha wateja wako wapate huduma nzuri na bora ambayo hawaipati sehemu
yoyote ila katika tovuti yako tu.Tovuti yako lazima iweze kuangalika kiurahisi
katika simu na vile vile kompyuta.
Hiki
ni kipengele cha mwisho kabisa katika kuhakikisha biashara yako inafanikiwa.Lazima
utangaze biashara yako ili uweze kupata wateja wengi siku hadi siku.Matangazo
ya biashara yako yatakuwezesha kujua changamoto zilizopo katika hiyo biashara
uliyoianzisha.Unapotangaza biashara yako tunazungumzia kutangaza tovuti
yako.Njia zipi utakazotumia kutangaza tovuti yako au kuongeza wateja.Ukiitangaza
tovuti yako itakuwezesha kujulikana kiurahisi kwa watu wenye mahitaji ya huduma
yako.Tangaza kupitia mitandao ya kijaamii vile vile itasaidia kuongeza idadi ya
watembeleaji wa kwenye tovuti yakio.Usipotumia mbinu sahihi katika kutangaza
tovuti yako basi itakuwa ni vigumu
katika kukamilisha malengo yako.Hili suala sio la kutilia shaka sana endapo unatoa
huduma iliyo na ubora ambao kila mtu anauhitaji.Utakapo toa huduma iliyo bora
basi itakuwa ni rahisi kuongeza idadi ya wateja maana watu wanatafuta huduma yako
iliyo bora sana kuliko nyingine.
Unafikiria
nini kuhusu kuanzisha biashara ya kimtandao ,andika maoni yako katika kisanduku
cha maoni.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni