tangazo

Uza/Nunua mifugo na vifaa vya ufugaji kuptia Mfugaji Marketplace

Jumamosi, 10 Machi 2018

KIJUE CHANZO CHA BIASHARA YAKO KUFA



Je ni biashara ngapi zinazoanzishwa na kufa kila mwaka?

Kwa wastani mfano zikianzishwa biashara 100 kwa mwaka basi biashara zitakazovuka mwaka ni chini ya 20.Hivyo kila mwaka 80% ya  biashara mpya zinakufa kabla ya kufikisha mwaka.

Je ni mambo gani yanayosababisha kufa kwa biashara kabla ya mwaka wa kwanza?

1.Elimu ndogo ya biashara.

"Mali bila daftari huisha bila habari", kukosekana kwa tarakimu na kumbukumbuku katika biashara ni jambo linalosababisha biashara kufa.Lazima ujue umeingiza shilingi ngapi na umetumia shilingi ngapi.Kukosekana kwa mapato na matumizi ndio mwazo wa kula mtaji bila kujua,wewe utaona biashara inaenda ila ukikaa kupiga hesabu utaona kuna kiashiria cha kupungua mtaji.

2.Kukosekana kwa moyo wa kijasiriamali.

Hili nalo ni tatizo kubwa,baadhi ya watu wanadhani wakianzisha biashara basi faida itapatikana kirahisi.Endapo kukawa na faida ndogo ukilinganisha na matarajio hapo ndipo mtu hukata tamaa,na ndio mwazo wa kufa kwa biashara. Jambo muhimu ni kwamba katika biashara yoyote lengo ni kupata faida,hata iwe ndogo kiasi gani ili mradi gharama za uendeshaji zinapatikana.

3.Kutomudu ushindani.

Ukishindwa kumudu ushindani uliopo ni tatizo kubwa.Endapo mwenzako anatengeneza bidhaa moja na wewe hakikisha bei yako iwe ndogo na uzidi ubora wake.Ukiwaza faida tu katika biashara yako hautoweza kumudu ushindani hivyo biashara yako ipo hatiani kufa.

4.Huduma mbovu kwa wateja.

Mapato makubwa utayapata ni jinsi gani unamhudumia mteja wako.Biashara yako inaweza kuwa nzuri ila tatizo likawa kwa wahudumu wako.Kinachotokea hapa ni kwamba mteja wako lazima ahame na kutafuta sehemu yenye huduma kwa wateja nzuri.Hapa tunazungumzia biashara ambazo 100% zinahitaji kutolewa na mhudumu na sio biashara za mtandao ambazo mara nyingi zinatumia automations.

5.Huduma mbovu bei kubwa.

Biashara kutoka China zinafanya vizuri kutokana na bei ndogo, japokuwa baadhi ya bidhaa zake sio bora.Wewe unachotakiwa kufanya ni kutoa huduma bora kwa bei ya chini,hapa kutakuwezesha kupata wateja wote wa kipato cha chini mpaka juu.Suala sio kuangalia faida kinachotakiwa kwanza ni kuua ushindani kisha kukuza jina.

6.Anza kuendesha biashara kitigitali.

Njia za kusaka wateja zinazidi kuwa tofauti tofauti.Ukitegemea mteja akufuate mpaka dukani mwenyewe mambo yanabadilika.Lazima uanze kujitangaza kwa njia za kidigitali kuweza kuvuta wateja wapya.Usipofanya hivyo wateja wapya utawapata kwa nadra na hata ulionao watapungua.Hapa ndipo mwanzo wa biashara yako kulegalega na hatimae kufa.Hakuna ujanja mwingine kwenye biashara zaidi ya kujipanga wewe mwenyewe na kujua unawavutiaje wateja.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Kufanya biashara ya samaki aina ya Degere

  1. Ufafanuzi Samaki aina ya degere ni sangara ambao wanakuwa na ukubwa ulio pungufu ya sentimeta 48 ambazo ndio ukubwa unaokubalika kisher...