Je utapeli unafanyika mitaani tu au
hadi mtandaoni ? ………..jibu ni NDIYO,
je ni kivipi?.Basi fuatilia Makala hii kwa undani ufahamu utapeli unavyofanyika
.Utapeli huu unafanyika kupitia mawazo ya kawaida ya biashara.Makampuni mengi
huwa yakimtamanisha mtu njia ambazo atazitumia na kupata peasa kwa haraka zaidi.Hapo
ndipo mtu hujikuta ametumbukia katika mikono ya matapeli.Utapeli katika mtandao
unashika kasi siku hadi siku.Makala hii itazungumzia aina moja ya utapeli unaofanyika katika matandao hususani
Tanzania.Hii itakuwezesha kuchukua njia thabiti za kuepukana nao vilevile
kushauri wengine kuhusu suala hili.
MAKAMPUNI YA UTAPELI KUPITIA MTANDAO
Je kuna makampuni nchini yanayofanya utapeli
bila ya serikali kujua au wananchi wake?
Kuna
makampuni nchini yanafanya utapeli na pengine wanaojiunga hawajui kuwa ni
utapeli tu.Makampuni ya aina hii nchi nyingi yameshapigwa marufuku na serikali
za nchi husika.kampuni la kitapeli utaligundua kwa ishara kuu moja ,hayana bidhaa za kuuuza.Makampuni haya
huwataka watu wajiunge kwa kiwango fulani cha pesa, na kila mtu yoyote
atakayeunganishwa na mteja , mteja huyo atapata kiwango fulani cha pesa.Mara
nyingi makampuni kama haya hutumia maneno tu kumshawishi mteja wao,kwa kila
unapoongeza mtu katika huo mtandao basi pesa yako ndiyo inavyoongezeka.
Kampuni kama forever living products siyo
la kitapeli maana wana bidhaa zao zinazo julikana na zipo wazi kabisa.Japokuwa
pia unaweza kupata kiwango fulani cha pesa unapoongeza mtu katika mtandao ila
bado sio la kitapeli kabisa.Kama ungependa kufanya biashara na hii kampuni ,basi jiunge nalo maana siyo la
kitapeli.Tafuta mtu unayemjua ambaye yupo katika kampuni hii akupe ushauri zaidi
namna ya kujiunga kama utapendelea.Kampuni jingine linalofanana na hili ni
trevo nalo si la kitapeli.Jinsi biashara inavyoendeshwa na kampuni la forever
living products inafanana na kampuni la trevo. Jiunge na makampuni haya kama
utapendelea .Ila uwe unajua jinsi ya kufanya
biashara(elimu ya biashara), maana kuwa na biashara na kufanya biashara ni
vitu viwili tofauti kabisa.Pasipo elimu muhimu ya biashara basi hutoweza
kuiendesha biashra yako na itakosa wateja.
Makampuni tunayozungumzia kuwa ni ya kitapeli
ni yale ambayo hayana bidhaa ya kuuza.Unajiunga
kwa kiwango fulani na kila utakaye muunganisha basi nawe utapata asilimia fulani
kutokana na huyo mtu uliye muunganisha.Inamaana ukijiunga ukakosa mtu wa kumuunga
inamaanisha hela uliyotoa imeenda bure, huu
ni utapeli.Fikiria kwa mfano mtandao ni wa watu wa nchini tu, na watu wote
wakajiunga je huo mtandao utaendelea
kukua?. Hii inamaanisha watu wasipojiunga basi na mtandao wote utapotea kabisa
na kufa.Mtandao ukifa na pesa yako imeenda na hakuna sharia ya kukuklinda wewe
uliyejiunga.Kupitia maelezo niliyoyatoa basi unaweza kutambua ipi ni kampuni ya
kitapeli na ipi siyo ya kitapeli.
Kabla ya kujiunga na kampuni yoyote inakubidi
ufanye uchunguzi wa kina kuhusu hiyo kampuni. Je ina tambulikas na serikali?
Ina bidhaa ya kuuza? Inafanyaje biashara yake?. Uchunguzi utakuwezesha kupata kampuni nzuri ambayo inaweza kukuongezea
kipato chako.Epuka makampuni yanayokuahidi kiwango kikubwa cha pesa utakapo
jiunga, hii huwa ni kivutio kupata wateja wengi.
Makala hii fupi imeandikwa kukupa muongozo
na sio kukushawishi ujiunge na makampuni
tajwa hapo juu.Hii ni kukuelewesha
makampuni ya kitapeli na yasiyo ya kitapeli endapo ukitaka kufanya
biashara nayo.Hivyo basi natumaini utakuwa umepata muongozo mzuri juu ya
makampuni hayo, kwa lolote basi usisahau kuandika maoni yako hapo chini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni