tangazo

Uza/Nunua mifugo na vifaa vya ufugaji kuptia Mfugaji Marketplace

Jumatano, 22 Aprili 2020

Biashara ya juisi za matunda

Kwa hapa kwetu Tanzania hii biashara wengi hawaitilii maanani sana na hata wale wanaoifanya wengi wao wanaifanya kawaida sana.
Ila hii ni biashara ambayo ukiwa serious na ukaamua kuifanya kwa kuzingatia kanuni zote unatengeneza faida kubwa.
Na biashara hii haihitaji mtaji mkubwa sana kwa kiasi cha M4 au 5 unaweza kufanya biashara hii ikawa ya kuvutia zaidi.

ZINGATIA HAYA.
Tafuta eneo zuri lililochangamka.
Kodi fremu na uifanye iwe nzuri na ya kuvutia zaidi.
Tafuta mashine za kutengeneza juice ya matunda.
Tengeneza juice ya matunda halisi bila kuchanganya na chochote kile.
Nunua matunda safi na mazuri achana na matunda mabovu na yaliyooza.

Hizi ni baadhi ya juice ambazo ukizitengeneza kwa ufasaha utapiga pesa.

KUMBUKA KUWA HUTAKIWI KUONGEZA MAJI KWA BAADHI YA JUICE.

Juice ya tende hii hutengenezwa kwa.
Kwa maziwa, tende na korosho au karanga pekee, (usiweke maji)

Juice ya tikiti maji pia hutakiwi kuweka maji hata kidogo.

Juice ya miwa 
Hii pia hutakiwi kuweka maji hata tone.

Juice ya nanasi: hii hutakiwi kuweka maji hata tone.

Juice ya embe, parachichi, pasion hizi unaweka maji kidogo sana yaliyochemshwa kisha kupozwa ili kulinda afya ya mnywaji kumbuka kuwa huweki sukari bali unatumia asali kiasi.
Kuna aina nyingi za juice ila nimeangalia zile ambazo zimezoeleka kwa wengi na mambo kadhaa ya kuzingatiwa ili kuleta radhaa ya tofauti kwa mtumiaji.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Kufanya biashara ya samaki aina ya Degere

  1. Ufafanuzi Samaki aina ya degere ni sangara ambao wanakuwa na ukubwa ulio pungufu ya sentimeta 48 ambazo ndio ukubwa unaokubalika kisher...