tangazo

Uza/Nunua mifugo na vifaa vya ufugaji kuptia Mfugaji Marketplace

Jumatano, 22 Aprili 2020

Biashara za mtaji chini ya laki moja

Ni mara nyingi sana vijana tumekuwa tukihangaika huku na kule kutafuta kipato ila wengi wetu tumekuwa tukiambulia kusema hatuna mitaji ya kutosha sasa leo nakuletea hizi biashara baada ya kufanya utafiti wa kina

1. Kuuza dagaa wabichi
Hii biashara inawahusu watu waishio kando kando ya ziwa hasa ziwa victoria. Kwa wenyeji wa Mwanza natambua wanaelewa vizuri hii kitu. Katika biashara hii unachohitaji ni tenga lako na mtaji usiozidi 50,000 hata kama huna baiskel utakodi kwa siku utalipia 1000 tu. Haina changamoto sanaa tofauti na aibu hasa kama wewe ni msomi itakupa shida mpaka kuizoea 

2. Kukaanga samaki na kuwauza
Ni biashara nyingine ambayo inaleta pesa mingi sana zaidi ya maelezo. Hapa mtaji hauzidi 100,000 lkn utapata faida zaidi 15000 kwa siku. Kijana changamkia fursa

3. Kutembeza maziwa maeneo ya mjini.
Aisee kijana hii ni zaidi ya biashara niliwahi kuifanya hapa Mwanza lkn niliacha coz nilienda masomoni liporudi nikawa naona aibu tena hapo ndipo huwa naamini kuwa Elimu ni kifungo cha Maisha

4. Kulangua mboga mboga na kwenda kuuza jumla sokoni pale saba saba. 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Kufanya biashara ya samaki aina ya Degere

  1. Ufafanuzi Samaki aina ya degere ni sangara ambao wanakuwa na ukubwa ulio pungufu ya sentimeta 48 ambazo ndio ukubwa unaokubalika kisher...